Acts 8:1-4

1 aNaye Sauli alikuwepo pale, akiridhia kuuawa kwa Stefano.

Kanisa Lateswa Na Kutawanyika

Siku ile kukatukia mateso makuu dhidi ya kanisa huko Yerusalemu, waumini wote isipokuwa mitume wakatawanyika, wakakimbilia Uyahudi na Samaria.
2 bWatu wacha Mungu wakamzika Stefano na kumwombolezea sana. 3 cLakini kwa habari ya Sauli alikuwa analiharibu kanisa, akiingia nyumba kwa nyumba, akiwaburuta wanawake na wanaume na kuwatupa gerezani.

Filipo Ahubiri Injili Samaria

4 dKwa hiyo wale waliotawanyika wakalihubiri neno la Mungu kila mahali walipokwenda.
Copyright information for SwhNEN